Tips

Watanzania, kwani Magufuli Aliwezaje?

Watanzania, kwani Magufuli Aliwezaje

John Pombe Joseph Magufuli (29 Oktoba 1959 – 17 Machi 2021) alikuwa rais wa tano wa Tanzania, akihudumu kuanzia 2015 hadi kifo chake mwaka 2021.

Na, nimeandaa makala hii fupi kujikumbukisha mambo machache kati ya mengi aliyokuwa akiyafanya wakati wa uongozi wake.

Advertisements

Tanzania imeanza tena kuwa ya uchungu!

Mambo hayaeleweki, shida za kijamii zinazidi kumzidia mtanzania. Hapo ndipo palipo nifanya nijuliulize maswali–

1. Alikuwa akifanyaje MAJI hayakuwa mgao?
Kama hali ilivyokuwa sasa.

2. Alikuwa akifanyaje UMEME haukuwa mgao?
Kama hali ilvyokuwa sasa.

3. Alikuwa akifanyaje miundo mbinu ika-taradadi na kukuwa kwa kasi?
Tofauti na sasa.

4. Aliwezaje kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati? (I have proof, this is a known fact) na baadae kuporomoka ndani ya miezi michache?

5. Alitumia mikakati gani na kuweza kuzuia chakula kwenye nje ya nchi? Mfumuko wa bei na nafaka (chakula) kupanda bei kiasi hiki?

6. Aliwezaje kupunguza kukopa (madeni yasiyo lazima) kutoka nchi za nje kwa asilimia kubwa kuliko sasa?

7. Kabla ya kifo chake, alituhaidia treni ya umeme, tukaelezewa itakavyo kuwa, ila tulicholetewa ni tofauti kabisa, sijui nini wapi tulipokwama?


Ni mengi tuliahidiwa ila baada ya kifo chake, kila jambo kinaenda tofauti. Sitaki kumzungumzia mtu yeyote, ila mimi kama kijana wa Kitanzania, in my 20s, naona kama tulielekeapo sipo.

Tunahitaji nguvu na umoja uliokuepo enzi za JPM akiwa madarakani uendelee ili tuweze kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati au zaidi.

Tanzania (ya viwanda) aliyokuwa akiiona hayati bado yawezekana kufikiwa, nguvu tunazo, utajiri upo, ila tu, tunahitaji viongozi wenye chachu ya mafanikio kama sisi raia na sio janja janja!

Ukweli ni kwamba,

Asilimia 80% tunakwamishwa na uongozi, sera zitolewazwo hazitekelezwi, na miaka mitano baadae huja kuombewa kura hizo hizo.

Nashindwa elewa nani mwenye kiu ya mafanikio (ya ki-nchi) hapa, system and raia tu!

Guys, tunahitaji viongozi wazalendo. Viongozi wanaoweka utaifa kwanza, na sio u-wao mbele. Wanaofikiria jinsi ya kuitetea nchi kimaendeleo na sio kuiteketeza.

Muda umefika wakuacha tabia za upigaji na ku-focus kwenye maendeleo. Wananchi bado maskini, japokuwa nchi yao ni tajiri.

Read next: Who is J.P Magufuli? Get to Know Him Here

”Unapopewa madaraka lazima uyabebe na uwajibike kwa kila litakalotokea. Nchi hii tumekabidhiwa wote kwa ajili ya kuwatumikia watanzania” – Hayati, Rais J. Pombe Magufuli

Mungu ilaze roho ya rais wetu pendwa, Joseph Pombe Magufuli mahali pema. Amen.

Advertisements

Leave a Comment